Skip to main content

Wakalimani

Ikiwa huweza kuelewa Kiingereza vizuri, ni muhimu sana umwambie Hakimu kwamba Kiingereza chako si kizuri na kuwa unahitaji mkalimani. Ikiwa kesi yako ni kosa la jinai au la ukatili wa nyumbani, Mahakama itapanga na kulipa mkalimani kwa ajili yako. Haitatokea siku ile ile. Itabidii uje tena siku nyingine ili hiyo iweze kupangwa. 

Ikiwa kesi yako ni jambo la kiraia (isipokuwa jambo la ukatili wa nyumbani), utahitaji kupanga na kulipa kwa mkalimani wewe mwenyewe.  

Wakati unapopata mkalimani, ni muhimu sana uelewe kwamba yupo kutafsiri lugha tu; yeye siyo mshauri wako wa kisheria. Pia ni muhimu kuelewa wakalimani wako huru na wana wajibu kwa Mahakama kutokuwa na upendeleo (yaani, kutochagua upande wowote, bila upendeleo na kufanya tu kazi yake kama mkalimani). Wakalimani wanaweza kuwepo kwenye chumba cha mahakama, au huenda kuwepo kwenye simu.