Skip to main content

Usajili

Usajili husimamia shughuli za Mahakama ya Mahakimu. Uko mahali falani katika Mahakama, mara nyingi uko karibu na ukumbi. Ikiwa huwezi kupata usajili, unaweza kuuliza mtu fulani anayefanya kazi Mahakamani kukuambia iko wapi. 

Wafanyakazi wa usajili wanaweza kuwasaidia watu wanaokuja Mahakamani kuelewa vipengele vingi vya mchakato wa Mahakama. Wanaweza kukupa maelezo zaidi kuhusu jinsi Mahakama inavyofanya kazi, kukusaidia kujua ambapo kesi yako inasikilizwa, na kusaidia na kufikia huduma za msaada. Usajili pia ni mahali ambapo hati nyingi za mahakama lazima ziwekwe saini na kuwasilishwa (au kuhifadhi faili), kama hati zinazohusu dhamana.  

Usajili hauwezi kukupa ushauri wowote wa kisheria au kukuambia kufanya nini katika kesi yako ya mahakama.