Kuingia Chumba cha Mahakama
Kutakuwa na watu wengine katika chumba cha mahakama. Chumba cha mahakama kimepangiliwa kutoa nafasi kwa wanasheria, watu wa umma, wafanyakazi wa mahakama, na washiriki wengine wa mahakama. Picha hii inakuonyesha mpangilio wa jumla wa chumba cha mahakama.
Mara nyingi, Mahakama ziko wazi kwa watu wote. Inamaanisha kuwa mtu yeyote wa umma anaweza kuingia Mahakamani wakati kesi inaposikilizwa. Muda mwingine Mahakama inakuwa imefungwa, kwa hivyo ni watu wanahusika katika kesi inayosikilizwa tu wanaruhusiwa kuwepo. Hii ni kwa sababu ya aina ya kesi inayosikilizwa. Hiyo ni mahitaji ya kisheria. Wakati Mahakama imefungwa, hutaweza kuingia chumba cha mahakama hadi Mahakama ikiwa tayari kusikiliza kesi yako.