Skip to main content

Huduma za Msaada

Pamoja na usaidizi wa kisheria na wakalimani, pia unaweza kupata usaidizi kutoka huduma nyingine za msaada. Hii itategemea na aina ya kesi yako ya mahakama pamoja na hali yako ya kibinafsi. 

Mahakama hutoa huduma zinazoweza kukusaidia katika kushughulikia na taratibu za mahakama. Orodha ya huduma hizi inapatikana kwa https://www.courts.qld.gov.au/services. 

Pia kuna aina nyingi tofauti za huduma za msaada za serikali na jamii. Huduma hizi nyingi ni bure bila malipo.  

Ikiwa unahusika katika uhusiano wa ukatili wa nyumbani kunapatikana huduma nyingi tofauti za msaada zinazojumuisha kupata usaidizi kwenda Mahakamani, kukupendekeza kwa malazi ya mgogoro na kupata msaada wa kipesa. Pia kuna msaada ikiwa unahitaji usaidizi wa kuacha kabisa tabia ya ukatili. Orodha kamili ya huduma za msaada inapatikana kwa https://www.courts.qld.gov.au/going-to-court/domestic-violence/support-services#.