Huduma Nyingine
Kwa kawaida Mahakama zina vyoo kila sakafu. Baadhi ya vyoo vinapatikana kwa watu wenye ulemavu. Pia kuna vyumba vinavyopatikana kwa matumizi ya jumla, kama vile kujiandaa kwa kesi yako. Ikiwa mtu mwingine anatumia mojawapo ya vyumba hivyo, basi huwezi kutumia chumba kile wakati ule ule.
Ikiwa una matatizo ya kusikia , kunaweza kuwa vifaa vinavyopatikana kukusaidia kusikia kinachosemwa, kama kifaa cha kitanzi cha kusikia. Ikiwa unafikiri utahitaji kitanzi cha kusikia, unapaswa kuwaambia wafanyakazi kwenye usajili, ambao wanaweza kukiandaa kwa ajili yako. Pia huenda kuweza kutumia kifaa cha kusikia cha kubebeka, kama tayari kipo kwenye chumba cha mahakama. Unaweza kuuliza wafanyakazi wa mahakama kuhusu hiki.