Maelezo Kuhusu Mahakama ya Mahakimu
Mahakama ya Mahakimu ni ngazi ya kwanza ya mfumo wa mahakama katika Queensland. Kuna Mahakama za Mahakimu katika maeneo takriban 130 tofauti katika Jimbo. Kesi nyingi za jinai na kiraia zinaanzia katika Mahakama hii kwa namna fulani.
Kesi husikilizwa na Mahakimu, ambao ni waafisa wa mahakama wanaoamua kesi hizi, ama kwa njia ya awali au kwa njia ya mwisho, kulingana na aina ya kesi. Hakuna baraza za wazee katika Mahakama hii.
Ikiwa huna haja ya kwenda Mahakamani lakini unahitaji kuweka hati kwenye usajili, basi tafadhali fuata alama za usajili ili kuwasilisha hati hizo. Usajili uko karibu na lango kuu la jengo la mahakama.
Usajili pia ni mahali unapoweza kuweka saini kwenye hati (kwa mfano hati za dhamana) na kupata nakala za amri zilizotolewa Mahakama. Kuna kanuni juu ya aina za hati unazoweza kupata kutoka usajili. Ikiwa huelewi michakato ya usajili, wafanyakazi wa usajili huenda kuweza kukusaidia.