Skip to main content

Ulinzi wa Mahakama

Baadhi ya Mahakama zitakuwa na uchunguzi unaohusiana na ulinzi. Ikiwa Mahakama ina ulinzi, kila mtu anayehudhuria Mahakama lazima apitie kwenye uchunguzi.  

Hii ni kwa ajili ya usalama wa watu wote katika jengo la Mahakama. Inamaanisha kuwa utahitaji kuweka vitu vyako, kama begi, kupitia kwenye mashine ya kutambua chuma. 

Pia utahitaji kutembea kupitia mashine ya kutambua chuma. 

Pengine, utahitaji kuchunguzwa kwa kifaa cha kushikwa na mkono na mlinzi wa usalama. 

Ikiwa watapata kitu ambacho hakiruhusiwi katika jengo la Mahakama kwako wewe, wanaweza kukichukua kutoka kwako, kutegemeana na kitu hicho.