Kuja Mahakamani Kama Shahidi
Ikiwa wewe upo kwenye Mahakama ya Mahakimu kama shahidi, unapaswa kuarifu mtu yule aliyeombe uje Mahakamani au kuarifu wasajili mara tu unapowasili kwenye nyumba ya mahakama. Huwezi kuingia chumba cha mahakama hadi ni zamu yako kutoa ushahidi. Inabidii usubiri kwa mtu aliyekuomba kuja Mahakamani kukukuta, na yeye atakusindikiza kwa eneo ambalo unaweza kusubiri.
Huruhusiwi kuzungumzia kesi na mashahidi wengine ambao wanawezakwa wanasubiri pia.
Wakati inapokuwa zamu yako, mwendesha mashtaka au mtu anayeitwa afisa wa huduma za mahakama atakuita kutoa ushahidi. Atakuongoza kwa sanduku la mshahidi, ambapo ni mahali katika chumba cha mahakama mashahidi wanapokaa. Utaulizwa kula kiapo au uthibitisho, ambayo ni ahadi muhimu kuwa unachosema kwenye chumba cha mahakama kitakuwa ukweli.
Lazima useme ukweli wakati unapotoa ushahidi. Kutosema ukweli katika Mahakama kunaweza kuwa uhalifu.