Skip to main content

Baada ya Kesi Yako Imesikilizwa

Ni nini kitakachotokea baada ya Hakimu amesikiliza kesi yako kitategemea kesi ni ya aina gani na Hakimu ameamua nini. Mara nyingi Hakimu ataeleza ni nini kitakachotokea kwa hatua ijayo, kama vile kama utapaswa kurudi tena Mahakamani na wakati gani, au fomu zipi utahitaji kujaza. 

Hakikisha unasikiliza kwa makini wakati wote wa usikilizaji wa kesi na zingatia kile Hakimu anachosema utahitaji kufanya baadaye. Inasaidia ikiwa una daftari na kalamu ili uandike anachosema Hakimu.