Baada ya Kuchunguzwa na Walinzi
Kujua mahali kesi yako itakaposikilizwa:
Mahakama zingine zina ubao wa taarifa ambao unaonyesha kesi za kusikilizwa kila siku. Ikiwa upo hapa kwa ajili yako, basi tafuta jina lako. Ikiwa upo hapa kwa niaba ya kampuni yako, tafuta kwa jina la kampuni yako. Kwa kawaida orodha itakuwa katika mpangilio wa alfabeti kulingana na jina lako la ukoo au jina lako kuu la familia, au jina la kampuni. Karibu na jina lako, utaona nambari ya chumba cha mahakama ambacho unatakiwa kwenda. Ni muhimu kwamba ufike mapema.
Ikiwa hakuna kibao cha notisi au huwezi kupata jina lako, umwulize mfanyakazi kukuambia mahali ambapo kesi yako ya mahakama inasikilizwa.
Kitu gani chan kufany kabla ya kasi yako kusikilizwa:
Mara baada ya kujua mahali ambapo kesi yako inasikilizwa, unaweza kusubiri nje ya chumba cha mahakama, au ndani yake. Kuna kesi nyingi tofauti zinazosikilizwa kila siku, za jinai na za kiraia. Huenda ukahitaji kusubiri kwa muda kabla ya kesi yako kusikilizwa.
Baadhi ya mahakama zina shughuli nyingi, na ni muhimu usikilize jina lako au jina la kampuni yako mara tu unapokuwa Mahakamani au jengo la mahakama. Kipaza sauti kinaweza kutumika katika jengo la mahakama. Ikiwa unasubiri nje ya chumba cha mahakama, unapaswa kuepuka kutumia vipokea sauti vya masikioni ili uweze kusikia jina lako likiitwa.
Ikiwa unaona utahitaji mkalimani wa kukusaidia kuelewa kinachokuwa kinasemwa katika kesi yako, kuna maelezo zaidi hapa.
Ikiwa huna mwanasheria anayekuwakilishi katika kesi yako na unataka mmoja, kuna maelezo zaidi hapa.